GST yashiriki Maones...
GST yashiriki Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma 2026
19 Jun, 2026
GST yashiriki Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma 2026

GST YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026

📍Dodoma, Viwanja vya Chinangali

Watumishi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wameshiriki Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo Juni 16, 2026 na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 23, 2026.

Katika maonesho hayo, banda la GST limetembelewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Selemani Mkomi, ambaye amepongeza na kushukuru ushiriki wa Taasisi hiyo katika maonesho hayo yanayolenga kuonesha huduma na mafanikio ya taasisi za umma kwa wananchi.

Aidha, GST inatumia maonesho hayo kutoa elimu kuhusu shughuli zake za utafiti wa jiolojia, ukusanyaji wa taarifa za rasilimali madini na mchango wake katika maendeleo ya Sekta ya Madini nchini.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo:
“Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.”