Mkurugenzi wa Utawal...
Mkurugenzi wa Utawala GST Awapongeza Watumishi ka Kufanya Vizuri Michezo ya Mei Mosi.
03 Jun, 2026
Mkurugenzi wa Utawala  GST Awapongeza Watumishi ka Kufanya Vizuri Michezo ya Mei Mosi.

MKURUGENZI WA UTAWALA GST AWAPONGEZA  WATUMISHI KWA KUFANYA VIZURI MICHEZO YA MEI MOSI

📍Njombe

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Shughuli za Uendeshaji wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Bi. Neema Mhagama, amewapongeza watumishi wa taasisi hiyo kwa kushiriki kikamilifu na kuonesha ushindani mzuri katika michezo mbalimbali ya mashindano ya Mei Mosi, yaliyofanyika mkoani Njombe.

Bi. Mhagama alitoa pongezi hizo Aprili 30, 2026 alipokutana na watumishi hao, akieleza kufurahishwa na nidhamu, mshikamano na ari waliyoionesha wakati wa mashindano hayo yaliyowakutanisha wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali wakishirikiana na Wizara.

Alibainisha kuwa ushiriki wao umeendelea kuitangaza vyema GST na kuimarisha uhusiano baina ya watumishi wa sekta ya madini, huku akisisitiza umuhimu wa michezo katika kujenga afya, kuimarisha ushirikiano na kuongeza ufanisi kazini.

Katika mashindano hayo, watumishi wa GST kwa kushirikiana na Wizara waliibuka washindi katika michezo kadhaa ikiwemo pool table pamoja na riadha, hususan mbio za wazee, wakionesha uwezo mkubwa na ushindani wa hali ya juu.

Aidha, aliwataka watumishi kuendeleza ari hiyo ya ushindi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na michezo, akisisitiza kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kuimarisha afya na mshikamano mahali pa kazi.