Serikali Kuongeza Ut...
Serikali Kuongeza Utafiti wa Kina wa Madini Mirerani
26 Aug, 2026
Serikali Kuongeza Utafiti wa Kina wa Madini Mirerani

Serikali Kuongeza Utafiti wa Kina wa Madini Mirerani

📍 Mirerani, Arusha

Serikali imeeleza mpango wa kufanya utafiti wa kina wa madini katika eneo la Mirerani, Arusha, hatua inayolenga kuongeza uelewa wa rasilimali za madini na kuchochea tija katika Sekta ya Madini nchini.

Akizungumza wakati wa ziara yake Mirerani, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kutenga asilimia 10 ya maduhuli yatokanayo na Sekta ya Madini kwa ajili ya kuimarisha utafutaji wa kina wa madini nchini.

Waziri Mavunde alisitiza umuhimu wa wachimbaji wote wa madini ya Tanzanite, hususan wachimbaji wa kati, kutumia teknolojia za kisasa katika utafiti na uchimbaji wa madini ili kuongeza ufanisi, usalama na tija katika shughuli zao.

Aidha, aliwataka wachimbaji hao kuwasilisha mpango wa hatua walizofikia katika shughuli zao za uchimbaji na utafiti ndani ya wiki mbili, ili Serikali iweze kufuatilia maendeleo na kutoa ushirikiano unaohitajika.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa muhimu katika kuimarisha matumizi ya teknolojia na taarifa sahihi za kijiolojia, kuongeza uzalishaji wa Tanzanite na kuhakikisha rasilimali hiyo ya kimkakati inanufaisha zaidi Taifa na wananchi