GST kujenga Maabara ya Kisasa jijini Dodoma, Kufanya Utafiti wa kina kufikia 50%. Waziri Mhe. Mavunde ameyasema hayo leo Aprili 24, 2024 jijini Dodoma katika kikao cha kujadili namna bora ya utendaji kazi kilichowakutanisha Watumishi wote wa GST.
Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde amewataka Watumishi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kuchapa kazi kwa bidii ili kutimiza Vision 2030, GST Kujenga maabara ya Kisasa Jijini Dodoma.
Kampuni ya PMM Tanzania Limited Handeni Mkoani Tanga inayomiliki mgodi wa Magambazi imeanza shughuli za uzalishaji madini ya dhahabu ambapo kuanzia Agosti 2024 mgodi huo unatarajiwa kuzalisha kilo 25 za dhahabu kwa mwezi.
Geological Survey of Tanzania (GST) ilifanya utafiti wa jiofizikia kwa undani ili kuelewa hali ya chini ya ardhi katika eneo lililopangwa kwa ajili ya kituo kipya cha kuhifadhia mkusanyiko wa taka za madini katika Mgodi wa Williamson Diamonds Limited (WDL).
Tanzania Yanadi Fursa za Madini Mkakati Korea Kusini na Asia.
Wekeza Kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo Ya Taifa na Ustawi wa Jamii
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Taasisi ya Jiolojia ya Finland (GTK) kwa ajili ya kushirikiana kufanya tafiti za miamba na madini pamoja na kubadilishana uzoefu katika teknolojia hususani kwenye shughuli za utafiti Machi 21, 2024.
Waziri wa Madini Mhe. Anthony P. Mavunde na Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba wameshuhudia jaribio la urushwaji wa Ndege Nyuki (Drone) angani kwa ajili ya utafiti wa miamba na madini hususan madini ya Kinywe, Nikeli, chuma na titanium katika Kijiji cha Utimbe kata ya Lupaso wilayani ya Masasi mkoa wa Mtwara.
Madini Indaba, 2024
Mwenyekiti wa Bodi ya GST Prof Ikingura, Katibu wa Bodi Dkt Mussa Budeba na Wajumbe Wengine Katika Kikao cha 17 cha Bodi Kilichofanyika Tarehe 19 Januari 2024 Katika Ukumbi wa Prof Mruma Dodoma Ambapo Mwenyekiti Ameitaka Menejimenti ya GST Kutekeleza Kwa Ufanisi "Vision 2030"