Prof. Ikingura Aongoza Kikao cha 18 cha Bodi ya GST
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia ya Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Prof. Justinian Ikingura amekiongoza Kikao cha kawaida cha 18 cha Bodi hiyo kwa ajili ya kupitia taarifa ya utekelezaji wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2023/24.
Bodi hiyo imefanya Kikao hicho leo Aprili 24, 2024 katika ukumbi wa Abdulkarim Mruma uliopo jijini Dodoma ambapo wajumbe wa Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya Taasisi hiyo wamehudhuria.
Aidha, katika kikao hicho hoja mbalimbali zimejadiliwa na kutolewa maelekezo kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi ili kuchochea ukuaji wa sekta ya madini na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Aidha, kupitia kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi, Fedha na Utawala CPA Constantine Mashoko amewasilisha taarifa ya Kamati hiyo ambapo Wajumbe wa Bodi hiyo walipata fursa ya kujadili na kutoa maelekezo kwa Menejimenti ya Taasisi hiyo.
Aidha, Bi Bertha Sambo ambaye aliwasilisha Taarifa ya Kamati ya Jiosayansi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ameipongeza Menejimenti kwa utekelezaji mzuri wa kazi ilizojipangia na kuitaka kuongeza juhudi na bidii katika utendaji kazi ili kuhakikisha Taasisi hiyo inafikia malengo iliyojiwekea.