Katibu Mkuu wa Madini Atembelea Banda la GST Kwenye Maonesho ya Madini Geita
22 Sep, 2025

Geita, Septemba 22, 2025
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametembelea Banda la GST katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita.
Katika ziara hiyo, Mhandisi Samamba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo. Viongozi wengi waliotembelea banda la GST ni pamoja na Dkt. Mussa Budeba Mtendaji Mkuu wa GST, Mwenyekiti wa Tume, Dkt. Janet Lekashingo, pamoja na Makamishna wa Tume, Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi.
GST kupitia maonesho hayo inaonesha na kutoa elimu kwa wadau kuhusu teknolojia na mashine mbalimbali zinazotumika kwenye utafutaji na uchenjuaji wa madini.