GST Yatoa Matokeo ya...
GST Yatoa Matokeo ya Utafiti wa Madini Mererani Mkoani Manyara
28 Jun, 2024
GST Yatoa Matokeo ya Utafiti wa Madini Mererani Mkoani Manyara

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imefanya wasilisho la matokeo ya majaribio ya utafiti wa Jiofizikia kwa njia ya kurusha ndege yaani "Airborne Geophysical Survey" kwa kutumia Ndege Nyuki (Drone) uliofanyika Mwezi Februari 2024 katika eneo la Mererani kwenye Kitalu C na D Mkoani Manyara.

Aidha, uwasilishaji huu umefanyika mbele ya Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga na Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeda kwa nyakati tofauti ambapo uwasilishwaji wa Kitalu C ulifanyika Juni 21 na Kitalu D umefanyika leo Juni 22, 2024