GST Yapokea Wasilish...
GST Yapokea Wasilisho la Utendaji Kazi wa Kampuni ya Barrick
04 Mar, 2024
GST Yapokea Wasilisho la Utendaji Kazi wa Kampuni ya Barrick

Utafiti waongezeka Mgodi wa North Mara na Bulyanhulu
 
Tafiti imefanywa na Wataalamu kutoka GST na Kampuni ya Barrick Tanzania
 
Kaimu Mkurugenzi wa Kanzidata wa Taasisi ya jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania GST Alphonce  Bushi, amepokea wasilisho la utendaji kazi wa Kampuni ya BARRICK Tanzania kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo.
 
Wasilisho hilo limetolewa leo Februari 22, 2024 katika Kikao cha 3 cha wataalamu wa Jiolojia  GST na wataalamu kutoka BARRICK   katika ukumbi wa Prof. Abdulkarim Mruma.
 
Naye, Meneja wa Uchunguzi Tanzania kutoka Barrick Leopold Byemelwa, ambaye pia ni muwasilishaji wa mada, amejibu swali kuhusu utofauti wa tabia za mwamba unaobeba aina za madini mbalimbali kitaalamu unaitwa (mwamba mbale), lililoulizwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kanzidata, amesema BARRICK wanafanya uchenjuaji wa mbale kwa kuzingatia tabia za mbale ya miamba hiyo ili kuepuka kuathiri mpango kazi wao kwa mwaka.
 
Amesema, Wanatumia utaalamu maalumu katika uvunjaji na Uchanganyaji wa kemikali zinazotumika kutenganisha Dhahabu na Madini mengine.
 
Aidha, Bw Byemelwa amesema kutokana na tafiti pamoja na uchorongaji uliofanyika hadi sasa unaonesha kuwa mgodi wa North Mara unatarajiwa kufikia kikomo ifikapo mwaka 2050 kwa upande wa Bulyanhulu unatarajiwa kufikia kikomo ifikapo mwaka 2037.
 
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Jiolojia Yusto Shine, amewapongeza kwa wasilisho zuri ambalo wataalamu wamejifunza mambo mengi.
 
Awali, Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Notka Banteze amewakaribisha wataalamu hao na kuwapongeza kwa kazi nzuri inayofanywa na Kampuni hiyo.