GST Yaendelea na Uta...
GST Yaendelea na Utafiti wa Jiolojia katika Visiwa vya Pemba - Zanzibar
19 Feb, 2024
GST Yaendelea na Utafiti wa Jiolojia katika Visiwa vya Pemba - Zanzibar

Katika kutekeleza mashirikiano (MoU) kati ya Wizara ya Madini Tanzania Bara na Wizara ya Nishati, Maji na Madini ya Zanzibar, Timu ya wataalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeendelea na utafiti katika Visiwa vya Pemba, hii ni baada ya kukamilisha kwa utafiti katika Visiwa vya Unguja mnamo mwishoni mwa mwezi Desemba, 2023.

Utafiti huu kwa sasa unaendelea kwa upande wa Pemba na unalenga kuchora ramani ya jiolojia ya Visiwa vilivyopo Zanzibar. Timu ya wataalam wa GST iliyopo Mjini Chake Chake - Pemba inashirikiana na Timu ya watalaam kutoka Zanzibar kuhakikisha ramani hii inaibua fursa mbalimbali za Kijiolojia ikiwemo rasilimali madini, vyanzo vya maji, vivutio vya utalii wa jiolojia, hali ya udongo na miamba, maeneo hatarishi kwa miundombinu ya ujenzi.