Dkt. Budeba Atembele...
Dkt. Budeba Atembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi Zake Kwenye Maonesho ya Madini Geita.
07 Oct, 2024
Dkt. Budeba Atembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi Zake Kwenye Maonesho ya Madini Geita.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Dkt. Mussa D. Budeba ametembelea banda la Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Wadau wa Madini kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili, mjini Geita tarehe 5 Oktoba 2024.

Katika  Banda la Wizara ya Madini alielezwa kuhusu  namna Wizara ya Madini inavyoandaa na kusimamia Sera na Sheria ya Madini pamoja na Kanuni zake pamoja na mikakati iliyowekwa katika kuhakikisha watanzania wananufaika na Sekta ya Madini.

Katika banda la Tume ya Madini elimu ilitolewa  katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.