Majukumu
Majukumu ya GST
 
1. Kumshauri Waziri juu ya masuala ya jiolojia;
 
2. Kukusanya, kuchambua, kutafasiri na kutunza takwimu na taarifa za jiosayansi (jiolojia, jiokemia na jiofizikia) ambazo ni muhimu katika kuleta ufahamu wa kuwepo kwa madini mbalimbali na namna bora za kutafuta madini;
 
2. Kutengeneza ramani za jiosayansi zinazoainisha uwepo wa aina ya miamba, madini na mazingira ya jiosayansi (geoscientific environment) katika sehemu mbalimbali za nchi yetu;
 
4. Kusambaza ramani, taarifa na takwimu kwa wadau ili ziweze kutumika katika sekta za uchumi na kukuza pato la Taifa;
 
5. Kufanya uchunguzi wa maabara kwa sampuli za miamba, madini, mchanga wa vijito, maji, mimea na udongo kwa ajili ya tafiti mbalimbali na kutoa huduma za maabara kwa wadau wa ndani na nje ya nchi. Pia, kufanya tafiti za jiosayansi na uchenjuaji wa madini;
 
6. Kuratibu majanga ya asili ya jiolojia na kutoa ushauri wa namna bora ya kujikinga na kupunguza athari zake. Majanga hayo ni pamoja na; Matetemeko ya ardhi; Milipuko ya volcano; Maporomoko ya ardhi na miamba;
 
7. Mionzi asilia; Gesi na kemikali zitokanazo na miamba; na Mashimo ya asili ya jiolojia (sink holes).
Kufanya tafiti za jioteknolojia na kutoa ushauri unaostahili katika masuala ya ujenzi wa miundombinu na makazi;
 
8. Kufanya tafiti za mazingira hasa yanayohusiana na uchimbaji wa madini na kutoa ushauri;
 
9. Kutoa ushauri kwa wachimbaji wadogo na wa kati katika kubaini umbile na aina ya mashapo husika, kutambua aina na ubora wa madini pamoja na njia bora ya uchenjuaji;
 
10. Kufanya uchunguzi wa madini katika sampuli mbalimbali na kutoa matokeo kwa maandishi kwa sampuli zinazotakiwa kusafirishwa nje ya nchi ili ziweze kupata vibali (export permits); 
 
11. Kutoa ushauri wa kitaalamu katika Sekta za Madini, Maji na Ujenzi kwa Serikali na Wananchi kwa ujumla;
 
12. Kutoa ushauri wa kitaalamu wa matumizi ya madini na miamba katika kukarabati udongo kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao katika Sekta ya Kilimo; 
 
13. Kukusanya, kuhakiki, kuhifadhi takwimu na taarifa zinazowasilishwa na wachimbaji pamoja na watafiti wa madini;  na
 
14. Kufanya majukumu mengine kama yatakavyopangwa na Serikali.