GST ni nini?
GST ni nini?

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ni taasisi ya utafiti chini ya Wizara ya Madini na ilianzishwa baada ya Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kupitia The Written Laws (Miscellaneous Ammendments) Act, Na. 7 ya Mwaka 2017. Taasisi hii imetokana na iliyokuwa Wakala wa Jiolojia Tanzania chini ya Wizara ya Nishati na Madini ya kipindi hicho tangu  Mwaka 2005. Wakala huu umetokana na Idara kongwe ya Serikali ya Kikoloni ya Mwingereza iliyojulikana kama Idara ya Jiolojia na ilianzishwa rasmi tokea Mwaka 1925. GST ni taasisi yenye uzoefu mkubwa katika masuala ya utafiti wa madini (mineral explorations) na uratibu wa majanga asili ya jiolojia Afrika Mashaiki na Kati.