Waziri wa Madini Mheshimiwa Dotto Biteko ambaye pia Mbunge wa jimbo la Bukombe azindua magari mapya sita kwa ajili ya Utafiti wa madini nchini yatakayo tumiwa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST). Uzinduzi huo uliudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Profesa Shukrani Manya, Katibu Mkuu wa Madini Profesa Simoni Msanjila, Kamishna Mhandisi David Mlabwa na watumishi Mbalimbali wa GST.