Leo Julai 5, 2021 Waziri wa Madini , Mheshimiwa Dotto Biteko ametembelea Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na kuzungumza na wataalamu wake walioshiriki katika maonesho hayo. Kupitia ziara hiyo, Waziri Biteko aliweza pia kupata maelezo juu ya matumizi ya vifaa mbalimbali vya Utafiti wa Madini vilivyopo katika banda hilo.

Vilevile, Mwenyekiti wa Bodi ya GST Profesa Justinian Ikingura leo ametembelea Banda hilo na kuzungumza na wataalamu wa GST ikiwa pamoja na kujionea jinsi GST ilivyojipanga kutoa elimu kwa Umma.

Sambamba na wageni hao pia, GST imepata fursa ya kutembelewa na Bilionea Saniniu Lazer , baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalam wa GST ameipongeza GST kwa kazi nzuri za ushauri juu ya inayoendelea kuifanya ya kuchochea uwekezaji katika Sekta ya Madini kupitia tafiti zake za uewepo wa madini nchini.