Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Leo tarehe 23/02/2020 ametembelea banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika maonesho ya kimataifa ya uwekezaji katika sekta ya madini yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Mhe. Majaliwa ameweza kupata maelezo mbalimbali juu ya taarifa za jiosayansi zinazopatikana GST kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa GST Dr. Mussa Daniel Budeba. Aidha, Dr. Budeba alimwelezea mhe. Wazir Mkuu kuhusu madini ya viwandani kama kinywe (graphite) yanavyoongezewa thamani na GST kwa kutengenezea vyungu (crucible) vya kuyeyushia sampuli za dhahabu. Vilevile, Dr. Budeba aliongeza kuwa GST imeendelea kuboresha huduma zake za maabara na kuweza kupata ITHIBATI katika uchunguzi wa sampuli za dhahabu kwa kutumia tanuru.

Mtendaji Mkuu wa GST akitoa maelezo kuhusu GST kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa