Na Samwel Mtuwa – Morogoro

Timu ya wataalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wakiongozwa na Mtendaji Mkuu Dkt Mussa Budeba mnamo Septemba 1, 2020 walifika katika wilaya ya Malinyi kijiji cha Misegese mkoani Morogoro kunakosadikiwa uwepo wa Madini ya dhahabu. Wataalam hao walifika katika eneo hilo kwa lengo la kukutana na wachimbaji wa eneo hilo na kufanya upimaji wa miamba pamoja na kuchukua sampuli za miamba kutoka katika kila duara lililochimbwa kwa ajili ya utafiti zaidi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa GST aliwashukuru wachimbaji hao wadogo kwa ushirikiano mzuri walionesha na kuhaidi kuwa sampuli zote zilizochukuliwa zitafanyiwa utafiti wa jiosayansi na kuletewa mrejesho wa majibu . Aidha kaimu Meneja wa mgodi huo Ismail Hanga aliwashukuru wataalam wa GST kwa kuweza kufika katika eneo hilo na kuamini ujio wa wataalam umewapa motisha ya kuendelea na uchimbaji.

Eneo la uchimbaji lipo katika umbali wa kilomita 25 kutoka Malinyi mjini likiwa na wachimbaji wadogo takribani 50 lenye maduara 13 yanayendelea kuchimbwa.

Pichani wataalam wa GST katika eneo la machimbo