Wadau mbalimbali wanakaribishwa katika Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwenye maonesho ya uzalishaji na uwekezaji sekta ya madini kuanzia tarehe 16 Septemba 2021 mpaka tarehe 26 Septemba 2021.
Kupitia maonesho hayo, GST imeendelea kuwaelimisha na kuwafahamisha juu ya masuala mbalimbali ikiwemo aina za madini na miamba inayopatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi, huduma zitolewazo na GST, na njia za kisayansi zinazotumika katika utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji Madini.