Wadau mbalimbali wametembelea Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) . Kupitia maonesho hayo, GST imeendelea kuwaelimisha na kuwafahamisha juu ya masuala mbalimbali ikiwemo aina za madini na miamba inayopatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi; huduma zitolewazo na GST; na njia za kisayansi zinazotumika katika utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji Madini.

Aidha, katika msimu huu wa Sabasaba GST inatoa huduma za utambuzi wa madini kwa kutumia vifaa vya kisasa vilivyopo katika Banda lake. Pia, ushauri wa namna bora ya kutafuta na kuchenjua madini unatolewa . Vilevile, Banda la GST linaonesha madini mbalimbali yanayopatikana nchini ikiwa pamoja na Madini pekee ya Tanzanite.

Kauli Mbiu ya Maonesho ya mwaka wa huu wa 2021 inasema “Uchumi wa Viwanda Kwa Maendeleo ya Ajira na Biashara Endelevu”