Mashindano ya Remote Sensing kutoka nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC Countries) yanafanyika kila mwaka nchini Botswana yakiwa yanadhaminiwa na Japan Oil, Gas and Metals Extration Corporation (JOGMEC). JOGMEC ni taasisi ambayo ipo kwenye serikali ya Japan ambapo wameweka kituo cha Remote Sensing nchini Botswana kwa ajili ya mafunzo na mashindano kwa ajili ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC Countries). Mashindano hayo yalianza tarehe 28 Octoba mpaka 01 Novemba, 2019 nchini Botswana mji wa Lobatse.
Mashindano hayo yalishirikisha nchi kumi na tatu ambazo ni Zimbabwe, Tanzania, Msumbiji, Angola, Zambia, Botswana, Malawi, Lesotho, Eswatini, AfrikaKusini, DR.Congo, Madagascar na Nambia. Nchi ya Tanzania iliwakilishwa na wataalamu watatu kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST). Wataalamu hao ni Hafsa M.Seif, Abbas H.Mruma na Maswi M.Solomon.
Dhumuni la mashindano hayo kupima uwezo wa ufahamu na jinsi ya kutumia (Remote Sensing) kwenye sekta ya madini. Wataalamu walipewa taarifa (data) ambazo ni Sensor Data (ASTER, LANDSAT, SRTM-DEM na PALSAR) na hizo taarifa zilichakatwa (Processed) kwa kutumia software ENVI, ArcGIS na QGIS. Baada ya kuchakata hizo taarifa kila nchi walipaswa kuandaa wasilisho (presentation) kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya kupewa alama za ushindi.
Kwa upande wa Tanzania mada ya mradi wetu ilikuwa inahusu ‘Detection of Indicator Minerals for Copper Ore Deposits by using Remote Satellite Data in Mpwapwa, Tanzania.
Kwenye mashindano hayo kulitakiwa kuwa na washindi wanne tu baada ya kufanyiwa tathimini na majaji kutoka nchini Japan (Dr Nobuaki Ishikawa- General Manager JOGMEC Botswana, Dr Kazuyo Hirose-General Manager, International Cooperation Dept.,Japan Space Systems na Dr Rentaro Shimizu- Assistant General Manager JOGMEC Botswana).
Washindi waliofanikiwa kushinda ni Tanzania, Zimbabwe, Namibia na AfrikaKusini. Kila mshindi walipewa kikombe na cheti.

Washiriki wa Tanzania kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) wakiwa na kikombe chao cha ushindi

Mashindano ya Remote Sensing yalikuwa na mafanikio makubwa sana kwa kutuwezesha kujifunza vitu vingi kutoka kwa washiriki wenzetu kutoka nchi mbalimbali. Tunapendekeza Remote Sensing iwe inatumika kwenye mambo ya sekta yetu ya madini na kuwawezesha wajiolojia kufahamu jinsi gani Remote Sensing ina umuhimu kutumika kwenye sekta yetu ya madini.
Nje ya mashindano, JOGMEC iliweza kutangaza wakufunzi (Instructor) wanne wapya wa Remote Sensing kwa Nchi za SADC ambapo watatu walitokea DR.Congo na moja kutoka Tanzania ambae ni Hafsa M.Seif. Wakufunzi hao wapya waliweza kutunikiwa vyeti vya udhibitisho.

Mkufunzi kutoka Tanzania (GST) akikabidhiwa cheti

Tunapenda kuishukuru Wizara ya Madini na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini kwa kutuwezesha kushiriki katika mshindano ya Remote Sensing katika nchi za SADC, hatimaye tumefanikisha kuilete ushindi Tanzania.

Hafsa M. Seif, Maswi M. Solomon na Abbas H. Mruma
07/11/2019