Taasisi ya jiolojia na Utafiti wa madini Tanzania (GST) inapenda kuufahamisha umma kwamba kupitia kituo chake cha Dodoma zilipo ofisi za GST tarehe 30/07/2019 majira ya saa 12:35:19 asubuhi limetokea tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.6 katika kipimo cha Ritcher ambalo kitovu chake kipo umbali wa kilomita 462.2 za GPS (Straight measured distance) nyuzi 314 kaskazini magharibi mwa jiji la Dodoma. Utafiti unaonyesha kwamba kina cha tetemeko (hypocenter) hilo ni kilometa 15 chini ya ardhi ambapo kitovu chake kipo ndani ya mto Isanga kielelezo namba 1. ulioko mpakani kati ya Mkoa wa Shinyanga na Mwanza.

Kielelezo Namba 1: Ramani ya satellite ikionyesha kitovu cha tetemeko la ardhi Shinyanga katikati ya mto Isanga
Kielelezo Namba 2: Kitovu cha tetemeko katikati ya mto Isanga, Shinyanga

Jioljia ya Eneo
Eneo ambapo tetemeko limetokea linaonekanna kwa upande wa kaskazini magharibi lina miamba ya banded iron formation, quartzite pamoja na granite. Upande wa magharibi pamoja na kusini magharibi eneo limezungukwa na miamba ya banded iron formation pamoja na conglomerate na kwa upande wote wa mashariki eneo hilo linaonekana kuzungukwa na miamba aina ya granodiorite, Kielelezo namba 3. Hata hivyo eneo lote la jirani kutoka kwenye kitovu limezungukwa na udongo pamoja na mchanga kwa kuwa kitovu hicho kipo katikati ya mto Isanga. Kutokana na kitovu hicho kuwa juu ya mchanga wa mto Isanga kielelezo namba 2 na kwa kuwa eneo hilo limezungukwa na aina tofauti za miamba kwa upande wa kaskazini magharibi na upande wote wa mashariki ni vigumu kuthibitisha aina ya mwamba msingi (Bed rock) uliopo chini ya kitovu cha tetemeko

Kielezo Namba 3: Ramani ya jiolojia QDS 47 iliyoboreshwa

Pamoja na tetemeko hilo kuwa na ukubwa wa 4.6 katika kipimo cha Ritcher ambalo ni tetemeko la kiwango cha kati utafiti wa njia ya satellite haukuweza kugundua uwepo wa mipasuko juu ya uso wa dunia. Hii inatokana na ukweli kwamba eneo hilo sio la muinuko ni eneo la chini ambalo limejaa udongo au mchanga (Alluvium/swamp/mbuga soil) kama linavyoonekana katika ramani ya Jiolojia (kielelezo na. 5).

Figure 4: Ramani ya satellite ya eneo la kitovu cha tetemeko

Tetemeko hilo limesikika katika mji wa Nzega, hata hivyo mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya kutokea kwa madhara katika maeneo hayo. Taasisi ya jioljia na utafiti wa madini Tanzania inaendelea kufuatilia na inawasihi wananchi waendelelee na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa tetemeko hilo tunaamini limetokea katika mwamba imara ambao ni Tanzania Craton.

IMETOLEWA NA;
TAASISI YA JIOLOJIA NA UTAFITI WA
MADINI TANZANIA

31/07/2019