Katika kuelekea kilele Cha wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni 17, 2022 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini MHE. Msafiri Mbibo amefanya ziara ya kikazi Katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu aliambatana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ambapo aliweza kutembelea katika Maabara za GST Kwa lengo la kujua kazi zinazofanyika.

Akiwa Katika Maabara pia alipata fursa ya kuongea na baadhi ya Watumishi waliokuwa Katika sehemu zao za kazi.

Mara baada ya ziara ya kutembelea Maabara alifanya kikao na wajumbe wa Menejimenti juu ya maswala mbalimbali ya Utendaji kazi.

Mapema kabla ya kikao Cha Menejimenti kuanza Mtendaji Mkuu wa GST Dkt Mussa Budeba alimkaribisha Naibu Katibu Mkuu azungumze na wajumbe.

Akiongea katika kikao Naibu Katibu Mkuu alimshukuru Mtendaji Mkuu wa GST kwa jinsi wataalam wake wanavyofanya kazi Kwa ubora, uwazi na uwajibikaji katika sehemu zao za kazi.

Kwa niaba ya Watumishi wote wa GST Naibu Katibu Mkuu aliendelea kuwaasa wajumbe hao kuwa kufanya kazi Kwa juhudi na maarifa ndio njia bora ya kufanikisha majukumu ya Taasisi pamoja na wizara nzima ya Madini.

Wakati wa ziara Naibu Katibu kuu aliweza pia kujionea mashine mbalimbali za kisasa jinsi zinavyofanyakazi za uchunguzi wa sampuli mbalimbali za miamba na Madini.

Naibu Katibu Mkuu aliweza pia kujionea jinsi mashine ya kisasa ikifanya kazi ya kutengeneza vyungu vya kuyeyushia sampuli za madini ya dhahabu.