Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dr Mussa Budeba leo tarehe 3/7/2020 ametembelea Banda la GST katika maonesho ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba.

Wataalam kutoka GST walitoa maelezo mbalimbali juu ya jinsi GST ilivyojipanga kutoa Elimu kwa wadau katika msimu wote wa Maonesho , hususani katika Elimu ya miamba, uchakataji wa madini, ikiwa pamoja na kuonesha vitabu na machapisho mbalimbali ya Jiosayansi.

Pamoja na kutembelea banda hilo Dr Budeba alipata fursa pia ya kutembelea mabanda mengine yaliyo chini ya Wizara ya Madini.