Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru leo tarehe 09 Machi, 2022 amekutana na watumishi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye Taasisi za Wizara ya Madini yenye lengo la kufahamu utendajikazi wa GST pamoja na kuzungumza na Watumishi.

Akiwa GST alitembelea sehemu mbalimbali za utendajikazi kama vile Kurugenzi ya Maabara na vitengo vyake, Kurugenzi ya Kanzidata ya Taifa ya jiosayansi Katika sehemu ya Maktaba ya kutunza kumbukumbu za taarifa za utafiti, lengo kubwa la ziara hiyo ni kujionea jinsi taasisi inavyofanya kazi.