Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), yaendelea kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya madini nchini katika maonesho ya wiki ya viwanda yanayoendelea katika mkutano mkuu wa 39 wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Katika maonesho hayo GST inatoa elimu juu ya kazi mbalimbali za utafiti wa jiosayansi kwa maana ya jiolojia, jiokemia, jiofikia, miamba na madini nchini ikiwemo madini ya viwandani, madini nakshi (Dimension Stone), elimu nyingine ni juu ya uwepo wa madini ya ujenzi nchini.
Sambamba na elimu hiyo GST ipo na machapisho mbalimbali ya vitabu vya utafiti wa jiosayansi kama vile kitabu cha Madini yapatikanayo Tanzania toleo la nne kitabu hiki kinaelezea uwepo wa madini kuazia ngazi kijiji, wilaya, Kata mpaka mkoa.
Zaidi ya wadau mia mbili (200) wameweza kutembelea banda la GST na kupata taarifa mbalimbali za upatikanaji madini na miamba nchini.

Pichani chini, wadau mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa wataalam ndani ya Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika maonesho ya Jumuiya ya nchi za maendeleo kusini mwa Afrika(SADC) yaliombatana na maonesho ya wiki ya viwanda.