Balozi wa kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Marekani Dkt. Sulemain Haji Suleiman amefanya kikao kazi na timu ya wataalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza kuhusiana na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini kwa upande wa madini mkakati kama vile Lithium , Nickel na Cobalt.


