TAARIFA KWA UMMA

UTEUZI WA WENYEVITI NA WAJUMBE WA BODI ZA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA YA MADINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemteua Prof. Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) tarehe 18/01/2019. Kufuatia uteuzi huo Waziri wa Madini Mh. Doto Mashaka Biteko, kwa mujibu wa Kanuni ya 3(1)(b)(c)(d) na (e) ya Kanuni ya The Mining (Geological Survey), amewateua wajumbe wa Bodi ya GST kama ifuatavyo:

 1. Prof. Abdulkarim Hamisi Mruma
 2. Bw. Emanuel Mpawe Tutuba
 3. Bibi Bertha Ricky Sambo
 4. Prof. Shukrani Manya
 5. Bw. David R. Mulabwa
 6. Bibi Monica Otaru

Wakati huo huo kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli kumteua Meja Jenarali (Mstaafu) Michael Isamuhyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Tarehe 6 Desemba, 2018, Waziri wa Madini Mh. Doto Mashaka Biteko, kwa mujibu wa Kifungu cha 6 cha Tamko la Serikali la kuanzishwa STAMICO la mwaka 1972 kama lilivyorekebishwa mwaka 2015, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya STAMICO:

 1. Bibi Evelyn Makala
 2. Bibi Janeth William Lupenelo
 3. Bw. Emmanuel Maduhu Subbi
 4. Bibi Prisca Lwangili
 5. Bw. Lucas Lumambo Selelii
 6. Bw. Abdul Razaq Ibrahimu Badru
 7. Bw. Leonard Chacha Kitoka
 8. Bw. Elias Mahwago Kayandabila

Wizara inawapongeza wote walioteuliwa.

Imetolewa na;

Prof. Simon S. Msanjila

KATIBU MKUU

25 Januari, 2019