Na. Samwel Mtuwa – GST.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Prof.Justinian Ikingula, alitembelea taasisi ya GST iliyo chini ya wizara ya madini kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinavyofanyika katika kurugenzi mbalimbali ndani ya taasisi.
Taasisi ya GST inakazi mbalimbali ambazo ni kukusanya, kuchambua, kutafasiri na kutunza takwimu na taarifa mbalimbali za jiosayansi (Jiolojia, Jiofizikia na Jiokemia) na za upatikanaji madini nchini.
Kutengeneza ramani mbalimbali za jiosayansi zinazoainisha uwepo wa aina mbalimbali za miamba, madini, na hali ya jiosayansi .
Jukumu lingine ni kufanya uchunguzi wa miamba na madini katika maabara kupitia sampuli mbalimbali kama vile miamba, udongo, maji na mimea.
Sambamba na hayo GST pia ufanya tafiti za uchenjuaji wa madini kutoka katika mbale ili kuongeza thamanai yake.
GST pia imepewa dhamana ya kutoa vibali yaani (export permits) kwa ajili ya kusafirisha sampuli za miamba, udongo, na sampuli zilizo katika hali ya vimiminika (core, cuttings, rocks sample, soil, fluid samples.)
Katika upande wa majanga ya asili ya jiolojia kama vile matetemeko ya ardhi , milipuko ya volkeno, maporomoko ya ardhi, na kutoa ushauri wa namna bora ya kujikinga au kupunguza athari za majanga haya.
Aidha Prof Justinian Ikingula aliweza pia kupata maelezo juu ya ushauri wa kitaalam unaotolewa kwa wachimbaji wakubwa na wadogo wa madini nchini ikiwa pamoja na sekta ya kilimo na ujenzi.
Katika ziara yake hiyo ya ndani aliweza kutembelea kurugenzi na vitengo mbalimbali ndani ya GST.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya GST Prof Justinian Ikingura mwenyekoti la kijivu akiwa katika Maabara ya GST na wataalamu wa Jiosayansi akiangalia moja ya mwamba aina ya Granite ulioboreshwa kwa ajili matumizi mbalimbali.

Prof. Justinian Ikingura aliyenyoosha kidole kwenye kompyuta akijadiliana jambo na kaimu meneja wa kitengo cha Maktaba na Makunmbusho ya Taifa ya Jiolojia Bi Hafsa Maulidi akisikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa Bodi.