Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Yokbeth Myumbilwa amebainisha kuwa matokeo ya utafiti wa kina wa jiosayansi uliofanywa na GST kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yanaonesha uwepo wa mbale za dhahabu kiasi cha tani 4,394,162 zenye wakia 45,773.40 (kilo 1,423.71) za dhahabu katika eneo la D-reef na tani 452,215 zenye wakia 1,831.92 (kilo 56.98) za dhahabu katika eneo la Kapanda.