Na Samwel Mtuwa –GST
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imezindua Baraza jipya la Wafanyakazi na kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili katika utendaji kazi wa taasisi , akizugumza katika Baraza hilo mgeni rasmi wa uzinduzi huo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, alisema kuwa ukuaji wa sekta ya madini unachangiwa na upatikanaji wa taarifa sahihi za utafiti wa jiolojia juu ya uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Akizungumzia kuhusu haki za wafanyakazi, alisema suala la kupanda vyeo ni haki ya mtumishi , hivyo watalaamu wanatakiwa kupand vyeo kwa wakati pindi wanapokizi vigezo vyao.
Aidha Nyongo aliwataka wafanyakazi kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi na kufuata maadili na kusisitiza kua serikali haitasita kumchukulia hatua mfanyakazi ambaye atashindwa kufuata sheria za utumishi wa umma.
Aliongeza kuwa serikali haitawavumilia watumishi wasiofanya kazi kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma ambayo ni kutoa huduma bora ,utii wa sheria, bidii ya kazi , kutoa huduma bila upendeleo, pamoja na kuwajibika kwa umma pamoja na matumizi sahihi ya taarifa.
Uzinduzi huo uliudhuriwa na zaidi ya watumishi hamsini kutoka taasisi ya jiolojia na utafiti wa madini Tanzania , chuo cha madini , wizara ya madini , TUGHE mkoa , kamishna msaidizi kutoka waziri mkuu anayeshughulika na kazi , vijana , ajira na walemavu.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na watumishi wa GST hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanya kazi la GST, waliokaa pichani ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Issa Nchasi, Kaimu Mtendaji Mkuu Bi. Yokbeth Myumbilwa, Kaibu Tughe Mkoa John Mchenya.
Picha ya pamoja ya watumishi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wakiwa na mgeni rasmi wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi, waliokaaa mbele kuanzia upande wa kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya GST Prof. Justinian Ikingura , Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu (DAHRM) wa wizara ya madini Issa Nchasi , Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Bi. Yokbeth Myumbilwa, Katibu TUGHE mkoa Dodoma John Mchenya, na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Madini.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akijadiliana jambo na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania , wakati wa uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi la GST.