Uratibu wa Majanga ya Asili

Wakala wa Jiolojia Tanzania (Geological Survey of Tanzania - GST) ni wakala wa Serikali uliopo chini ya wizara ya Nishati na Madini na ulianzishwa rasmi mwaka 2005. Baadhi ya majukumu yake ni kufanya tafiti zinazolenga kubaini uwepo wa madini katika sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania. GST kwa niaba ya Serikali ni mhifadhi mkuu wa taarifa zote zinazohusu upatikanaji wa madini hapa nchini (geo-scientific data & information). Aidha, GST ina jukumu la kuratibu majanga ya asili ya kijiolojia kama vile matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkeno, maporomoko ya ardhi na gesi za sumu pamoja na mionzi itokayo ardhini

Download

Read